Kifo cha Kim Jong Nam Usalama waimarishwa hospitali ulikohifadhiwa mwili wake

Usalama umeimarishwa kuulinda mwili wa Kim Jong Nam aliyeuawa mwishoni mwa wiki nchini Malasysia ambapo Polisi wenye silaha nzito leo wamewasili katika hospitali ambako mwili wake umehifadhiwa. Marehemu Kim Jong Num ambaye ni kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini aliuawa kufuatia shambulizi akiwa uwanja wa ndege wa Kuala Lumpa. Wizara ya mambo ya nje ya[…]

Zaidi ya watu 100,000 wanakabiliwa na njaa maeneo yaliyokumbwa na mapigano Sudan Kusini

Zaidi ya watu 100,000 wanakabiliwa na njaa katika maeneo yaliyokumbwa na mapigano Sudan Kusini, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa serikali ya Sudan Kusini pamoja na taarifa iliyotolewa leo na mashirika matatu ya kimataifa. Kwa mujibu wa mashirika hayo ambayo ni pamoja na shirika la chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), shirika linaloshughulikia masuala ya[…]

Mapambano dhidi ya dawa za kulevya Mkuu wa Wilaya ya Muheza aomba ushirikiano kwa wananchi

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuwafichua wanaojihusisha na uuzaji usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya. Wito huo ameutoa wakati akihutubia wananchi wa katika hafla ya uzinduzi wa visima viwili vya maji katika kata ya Bwembwera na kijiji cha kwakifua wilayani muheza .[…]

Mahakama Kuu kanda ya DSM leo imetoa zuio la kutomkamata au kuwekwa kizuizini Freeman Mbowe

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam leo imetoa zuio la kutomkamata Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Freeman Mbowe mpaka maombi aliyowasilisha ya kuomba kutokukamatwa na kuwekwa kizuizini yatakaposikilizwa na kutolewa maamuzi. Zuio hilo limetolewa na jopo la majaji mahakamani hapo ambapo maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na[…]