APRM imebaini mafanikio makubwa eneo la kuimarisha demokrasia, usimamizi wa uchumi na huduma za kijamii.

Mpango wa tathmini ya utawala bora katika Bara la Afrika APRM umebaini kuwepo kwa mafanikio makubwa hapa nchini katika eneo la kuimarisha demokrasia, usimamizi wa uchumi na huduma za kijamii.

Aidha mpango huo unatajwa kufanya vema katika maeneo mengine yakiwemo ya uendeshaji wa mashirika ya biashara ambapo Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika eneo la usimamizi wa rasilimali ya ardhi na madini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wataalam wa kutathmini mpango huo ulioanzishwa miaka 16 iliyopita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, amesema mpango huo pamoja na mambo mengine umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa katika usimamizi wa utawala bora hapa nchini.

Kwa upande wake Mtaalam wa masuala ya kutathmini utawala bora APRM Dkt. Rehema Twalib amesema miongoni mwa maeneo yanayoifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano ni pamoja na ilivyofanikiwa kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar, sera nzuri za uchumi, mipango ya maendeleo na ukuzaji wa Biashara hususan kwenye sekta Binafsi na hivyo kutambulika miongoni kwa nchi 33 zinazotekeleza Mpango huo Afrika.

APRM ni Mpango wa tathmini ya utawala bora katika Bara la Afrika wenye lengo la kuangalia namna zinavyotekeleza masuala ya utawala bora na kuimarisha huduma za Jamii kwa raia.

Comments

comments