Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama wameendelea kukamata bidhaa za Vyakula na Mafuta zinazoingizwa kupitia bahari ya Hindi katika ukanda wa Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Madumu 275 ya Mafuta ya Kula yaliobandikwa lebo yakionesha yanatoka nchini Malaysia pamoja na mifuko ya Sukari inayoonesha inatoka nchini Msumbiji,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ameendelea kuwatahadharisha wananchi kuwafichua wale wanaoendesha vitendo hivyo haramu. Aidha Chongolo amesema waingizaji hao wa bidhaa hizo zisizolipiwa kodi na Ushuru ambazo usalama wake kwa matumizi ya binadamu[…]

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesisitiza haja ya nchi za Afrika Mashariki kushirikiana katika sekta ya afya kwa manufaa ya wakazi wa ukanda wote wa Afrika Mashariki.

Aidha amesema huwezi kuzungumzia Tanzania kufikia uchumi wa kati bila kuzungumzia uboreshaji wa afya za watu wake. Makamu wa rais ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati anafungua kongamano la afya na sayansi la Afrika Mashariki ambalo limekutanisha wataalamu wa afya, wanasayansi , mawaziri wa afya, watafiti na wadau wa afya kutoka Afrika mashariki na[…]