Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU imewaonya wananchi pamoja na watumishi wa Umma, na Serikali kujiepusha na Vitendo vya Rushwa, Utakatishaji fedha pamoja na Ufisadi kwani hivi sasa wana Mamlaka kamili ya Kutaifisha Mali za Watuhumiwa pindi Watakapothibitika wamejihusisha na Vitendo hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema kutokana na sheria hiyo wananchi na watumishi wa Umma na serikali wanatakiwa kuchukua tahadhari. Kamishna Diwani amesema Takukuru kuanzia mwaka 2016-2019 imeingiza shilingi Billioni 14.9 kwa kutaifisha Mali za wala[…]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha akiwa ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali William Kalaghe pamoja na Afisa Masoko wa NBC Neemarose Singo. Share on: WhatsApp

Baadhi ya wavuvi katika bwawa la MWANZUGI wilayani Igunga baada ya kupatiwa elimu ya uvuvi na shirika la kimataifa la Heifer kupitia mradi wa Igunga Eco Village wamelalamikia wataalamu wa uvuvi wanaosimamia bwawa hilo kwa madai ya kushindwa kuwapa ushirikiano wa kutosha.

Miongoni mwa shughuli zinazofanya katika mradi wa Igunga eco village ni pamoja na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za uzalishaji kitaalamu ambazo haziathiri mazao ya misiti ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi. Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwa ameambatana na wataalamu mbalimbali anafika katika bwawa hili na kupokea malalamiko kutoka kwa wavuvi. Hata hivyo Upande[…]