Wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki wilayani Arumeru wametakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi ambao watajitolea kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wakazi wa jimbo hilo ambalo bado lipo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na viongozi wa mila wa kabila la wameru maarufu kama washili kwa lengo la kujadili ni kwa namna gani wananchi hao wameupokea uamuzi wa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kumfutia ubunge , mbunge wao Joshua Nasari. Mmoja wa viongozi maarufu jimboni humo generali mstaafu Merisho[…]

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa Stigler’s Gorge wilayani Rufiji mkoani Pwani imeelezea kuridhishwa na hatua za awali za utekelezaji mradi huo.

Katika eneo hilo kamati hiyo imejionea kazi za miundombinu-wezeshi ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na nguzo za umeme kwenye mradi huo ambao unaratajiwa kutumia zaidi ya shilingi trilioni 6.5 na kuzalisha umeme megawati 2,115 utakapokamilika. Akiongea mara baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya madini na nishati kutembelea eneo la mradi wa kuzalisha umeme[…]

Kufuatia malalamiko ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam kuhusu ugumu wa usafiri huo, serikali imeingilia kati ili kupata ufumbuzi wa haraka wa kukabiliana na hali hiyo huku ikisema imeunda timu maalumu inayofanya mapitio ya namna bora ya kuboresha mradi huo.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa – TAMISEMI Seleman Jaffo amemwagiza mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka – DART Mhandisi Leornard Lwakatare ahakikishe kwamba mabasi 10 yanayofanya safari za kimara – Mbezi kuyahamishia Kimara – Kivukoni na Gerezani ili kuwapunguzia abiria adha inayowakabili. Katika kukabiliana na[…]

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaendesha Kampeni ya kutoa elimu nchi nzima kwa vijana ili vijana hao waweze kukuza vipaji vyao pamoja na kuwa na weledi katika utengenezaji wa picha za filamu.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo katika Mji mdogo wa Nduguti,wilayani Mkalama baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo iliyoonyesha jitihada za kulikarabati jengo la Boma la Mjerumani na kubaini pia kuwa wilaya ya Mkalala bado ipo nyuma katika masuala ya utengenezaji wa picha za filamu na ndipo akatoa ahadi kwa wana – Mkalama. Aidha Dkt. Mwakyembe[…]

Watu Arobaini na tisa wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyotokea katika misikiti miwili Christchurch nchini New Zealand.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameelezea tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi na ni tukio baya kuikumba nchi hiyo. Maafisa wa polisi nchini humo wamesema wanaume watatu na mwanamke mmoja wanashikiliwa kuhusika na shambulizi hilo na kuonya kuna uwezekano wa kuwepo kwa watuhumiwa wengine zaidi. Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema[…]