Kamati ya Saa 72 inayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara yailima faini ya milioni Sita Yanga pamoja na Kutoa Onyo kali kwa Makocha wa Vilabu Vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara kwa utovu wa Nidhamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amewataka makocha ambao wanashambulia waamuzi wapeleke ushahidi ndani ya shirikisho la soka TFF kwaajili ya hatua zichukuliwe na vyombo vinavyoongoza shirikisho hilo. Aidha Wambura ameainisha adhabu kwa timu za Simba,Yanga na Azam Fc ambazo zilikiuka utaratibu wa kisheria kwa kutotumia milango rasmi[…]

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Kampala, Uganda kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’ unaotarajiwa kufanyika kesho na kesho kutwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Kampala, Uganda kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika kesho na keshokutwa. Makamu wa Rais atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mkutano huo. Katika Uwanja wa Ndege[…]

Serikali ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba imewatoa hofu wananchi kwamba dawa za malaria zinazopigwa majumbani mwao hazina madhara kwao, bali zimelenga kuangamiza mbu wanaoeneza malaria.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi Salama Mbarouk Khatib wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Tumbe ambao wamegoma kupigiwa dawa majumbani mwao. Amesema lengo la serikali ni kutokomeza ugonjwa wa malaria ambapo ameahidi kusimamia zoezi hilo ili kuhakikisha linafanikiwa na nyumba zote zinapigwa dawa. Afisa kutoka kitengo cha Malaria wizara[…]

Msemaji wa shirika la ndege la Ethiopia amesema ndege zote za shirika hilo chapa Boeing 737 Max 8 hazitaruka kama hatua ya tahadhari, kufuatia ajali ya moja kati ya ndege zake iliyoua watu zaidi ya 157.

Bwana Asrat Begashaw amesema leo kwamba licha ya kwamba haijafahamika kile kilichosababisha ajali hiyo jana, shirika hilo limeamua kutorusha ndege zake nyingine chapa 737 Max 8 hadi taarifa nyingine itakapotolewa, ikiwa ni kuchukua tahadhari zaidi. Mamlala ya safari za anga nchini China pia imeamuru mashirika yote ya ndege nchini humo yasirushe ndege zake za Boeing[…]

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bw. Mussa Sima amesema ameridhishwa na utunzwaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji vinavyoelekea katika Bonde la Mto Rufiji na kuagiza mamlaka husika kuendelea kuvilinda kwa gharama zote.

Akizungumza katika eneo utakapojengwa mradi wa umeme wa ‘Stigler’s Gorge’ akiambatana na wajumbe Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) iliyokwenda kujionea namna mradi huo utakavyotekelezwa pasipo kuleta athari zozote za kimazingira, Waziri Sima amesema ziara yake ya kukagua na kuangalia vyanzo vya maji maeneo mbalimbali[…]

Washtakiwa watatu wa makosa ya mauaji ya watoto Njombe wamefikishwa mahakamani na kesi yao kutajwa kwa mara tatu na kisha kuahirishwa hadi Machi 25 Mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Washtakiwa watatu wa makosa ya mauaji ya watoto GODLIVER, GILIAD na GASPER NZIKU waliokuwa wakazi wa Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa wilaya na mkoa wa Njombe wanaokabiliwa na kesi namba moja ya mwaka 2019 leo wamefikishwa mahakamani na kesi yao kutajwa kwa mara tatu na kisha kuahirishwa hadi Machi 25 Mwaka huu kwa kuwa[…]

Siku moja baada ya ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines kuua watu 157 kutoka zaidi mataifa 30, serikali ya Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja.

Raia 32 wa Kenya ni miongoni wa abiria wote 157 waliopoteza maisha kufuatia ajali hiyo ya ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya. Ajali hiyo ilitokea mapema jana majira ya asubuhi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa. Taarifa ya awali[…]

Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019).

Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019) yenye lengo la kutaka kufahamisha wananchi hasa wa Dodoma nini taasisi hizo zinafanya sambamba na kujua fursa zilizopo katika Taasisi hizo na[…]