Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano imewaagiza mafundi simu nchini, kujisajili katika Ofisi za Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kudhibiti uhalifu unaofanyika kwa njia ya mitandao.

Kilio kikubwa kwa Watanzania wengi hivi sasa ni kupokea ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi, kutoka kwa baadhi ya matapeli wakiomba kutumiwa fedha kama njia ya kujikumu kimaisha. Kutokana na wimbi hilo Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Atashasta Nditie, hapa anakutana na Chama cha mafundi simu mkoa wa Mwanza, ili kutafuta[…]

Jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM mkoani Pwani -UWT-wameadhimisha Siku ya Wanawake duniani kwa kupaka rangi mnara wa bibi Titi Mohammed ikiwa ni ishara ya kumuenzi mwasisi huyo wa CCM kwa upande wa wanawake nchini.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani wanawake wa mkoa wa Pwani CCM wameazimisha Siku hiyo katika kijiji cha mkongo kata ya mkongo wilaya Rufiji ambapo pamoja Na shughuli nyingine wametumia fursa hiyo kungarisha mnara huo uliojengwa….ikiwa ni ishara ya kumuenzi mwanasiasa hiyo mkongwe aliyekuwa miungoni mwa viongozi wa awamu ya kwanza waliopigania Uhuru wa nchi.[…]

Jumla ya abiria 950 waliokuwa wanaosafiri na meli ya MV Sea Star 1 kutoka bandari ya Wete kwenda Unguja wamekwama kuondoka kwa muda baada ya kutokea hitilafu ya umeme ndani ya meli hiyo.

Baadhi ya abiria akiwemo Ali Hossein, Shehe Jamali na Halma Ali wameipongeza hatua zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi katika kuokoa maisha yao, na kuushauri uongozi wa meli kufanya ukaguzi kabla ya meli haijaanza safari. Nahodha wa meli hiyo Nassor Abubakar amesema hakuna tatizo kubwa lililojitokeza na kusema kuwa meli itaanza safari baada ya ukaguzi kufanywa[…]

Rais Dk. John Pombe Magufuli amesema licha ya Jeshi la polisi nchini kufanya kazi nzuri bado zipo dosari ndogo ndogo zinazoharibu taswira nzuri ya jeshi hilo ikiwemo baadhi ya watendaji kukosa uadilifu na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini dar es salaam mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kiapo kwa mawaziri wawili walioteuliwa mwishoni mwa wiki, balozi mmoja pamoja na makamishna watano wa Polisi ambao wamevalishwa vyeo. Amesema yapo baadhi ya matukio ya uhalifu ambayo Jeshi la polisi limeshindwa kuchukua hatua licha ya uthitisho wa awali[…]