KAMISHENI YA UTALII KUTOA ELIMU YA HISTORIA YA UTALII ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amesisitiza haja ya Kamisheni ya Utalii kutoa elimu ya historia ya Utalii hapa Zanzibar ili kuujua unakotoka na unakokwenda na hatua zilizofikiwa hivi sasa katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar. Dk. Shein aliyasema hayo leo, alipokutana na uongozi wa Wizara ya Habari,[…]

RAIS WA VENEZUELA AMPIGA MARUFUKU JUAN GUAIDO KUSHIKILIA WADHIFA WA UMMA

Utawala wa rais wa Venezuela Nicoals Maduro, uliotiwa nguvu na hatua ya Urusi kupeleka wanajeshi wake nchini humo, umetangaza kumpiga marufuku kiongozi aliyejitangaza wa mpito Juan Guaido ambaye anaungwa mkono na Marekani, kushikilia wadhifa wa umma. Lakini spika huyo wa Bunge la Venezuela akajibu maramoja kupinga uamuzi huo unaomzuia kwa miaka 15 ambao ulitangazwa kwenye[…]

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Mbeya kutibu magonjwa ambayo yameshindikana mahali pengine.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ‘UDSM’ na Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi ambacho kinatarajiwa kujengwa Mkoani Mbeya, kinatakiwa kuwa chuo cha mfano ambacho kitazalisha wataalam wenye ujuzi mkubwa pamoja kutibu magonjwa ambayo yameshindikana mahali pengine . Akiwa[…]

Kampuni ya Uhuru Media Group kuzindua Jukwaa la Tafakuri linalolenga kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Kampuni ya Uhuru Media Group inatarajia kuzindua Jukwaa la Tafakuri linalolenga kujenga taifa na kulinda uhuru kwa kuwarithisha vijana uhifadhi wa historia ,utamaduni na rasilimali za nchi na za Afrika kwa ujumla uzinduzi ambao utafanyika machi 30 mwaka huu eneo la Mlimani City katika ukumbi wa Cinemax jijini Dar es salaam. Akizungumza jijini Dar es[…]

Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) atoa ufafanuzi kuhusu hatma ya watu wanne kati ya kumi na wawili wa kesi ya uhujumu uchumi.

Baada ya hukumu ya watu wanne kati ya kumi na wawili wa kesi ya uhujumu uchumi kuibua maswali kuhusu hatma ya washitakiwa wanane waliokana mashitaka tisa ya kesi hiyo, mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, leo ametoa ufafanuzi kuhusu hatma yao. Washitakiwa wanane waliosalia katika kesi hiyo, baada ya kukamatwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza[…]

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama wameendelea kukamata bidhaa za Vyakula na Mafuta zinazoingizwa kupitia bahari ya Hindi katika ukanda wa Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam

Madumu 275 ya Mafuta ya Kula yaliobandikwa lebo yakionesha yanatoka nchini Malaysia pamoja na mifuko ya Sukari inayoonesha inatoka nchini Msumbiji,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ameendelea kuwatahadharisha wananchi kuwafichua wale wanaoendesha vitendo hivyo haramu. Aidha Chongolo amesema waingizaji hao wa bidhaa hizo zisizolipiwa kodi na Ushuru ambazo usalama wake kwa matumizi ya binadamu[…]