Watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja mkoani Njombe yaliyotokea Januari 20 mwaka huu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe na kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Joel Joseph Nziku mwenye umri wa miaka 35, Nasson Alfred Kaduma miaka 39 na Alphonce Edward Danda miaka 51. Akisoma mashtaka yanayowakabili mbelea ya hakimu mkazi Magdalena Ntandu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe , Mwanasheria Mwandamizi wa serikali, Ahmed Seif amesema watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu ya mauaji[…]

Watanzania wamehimizwa kuthamini lugha ya Kiswahili ili kudumisha utamaduni wa mtanzania pamoja na kuitangaza lugha hiyo katika mataifa mengine.

Watanzania wamehimizwa kuthamini lugha ya Kiswahili ili kudumisha utamaduni wa mtanzania pamoja na kuitangaza lugha hiyo katika mataifa mengine ili iweze kufahamika zaidi na kutumika kama lugha kuu ya mawasiliano. Akizungumza wakati akizindua mwongozo wa kufundishia lugha ya Kiswahili kwa wageni wanaotoka nje ya nchi pamoja na ufungaji wa mafunzo ya kuongeza standi za kufundishia[…]

Balozi wa Sweden pamoja na Balozi wa Algeria nchi Tanzania wameelezea kuridhishwa na mwenendo wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na Ufisadi.

Balozi wa Sweden pamoja na Balozi wa Algeria nchi Tanzania wameelezea kuridhishwa na mwenendo wa serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na Ufisadi pamoja na katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo Elimu, Afya na Maji. Akizungumza na Channel Ten mara baada ya mazungumzo na balozi wa Sweden Andres Sjoberg katika Ofisi[…]

Waziri Angela Kairuki amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa Wawekezaji na Wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa Wawekezaji na Wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuhakikisha vikwazo vilivyokuwa vinawakabili ikiwemo urasimu katika utoaji vibali na upatikanaji wa ardhi vinatokomezwa. Waziri Kariuki pia ametoa rai kwa Watanzania wenye maeneo makubwa ya ardhi[…]

Katika kuelekea uchumi wa kati mwaka 2025, Shirika la viwango Tanzania (TBS), limeanza kutoa elimu ya uanzishaji wa viwanda vidogo na uboreshaji wa bidhaa, ili kuwawezesha wajasiriamali nchini kuhimili ushindani wa kibiashara.

Katika kuelekea uchumi wa kati mwaka 2025, Shirika la viwango Tanzania (TBS), limeanza kutoa elimu ya uanzishaji wa viwanda vidogo na uboreshaji wa bidhaa, ili kuwawezesha wajasiriamali nchini kuhimili ushindani wa kibiashara katika soko la ndani na nje ya nchi. Akizungumzia suala hilo Jijini Mwanza kaimu mkurugenzi wa Shirika hilo Lazaro Msasalaga, amesema (TBS) imeona[…]

Polisi wamesema watu kumi na saba wamepoteza maisha kufuatia janga la moto uliotokea katika hoteli moja mjini Delhi nchini India mapema leo asubuhi.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema waliopoteza maisha ni pamoja na mwanamke na mtoto ambao walijaribu kuruka kutoka kwenye dirisha kutafuta kuokoa maisha yao. Maafisa wa India wamesema watu thelathini na watano ameokolewa, huku wengine majeruhi wakifisikishwa hospitali. Hoteli hiyo ya Arpit Palace ipo katika eneo la Karol Bagh, maarufu kwa watalii kutokana na kuwa na[…]

Upinzani nchini Venezuela unapanga maandamano zaidi leo kushinikiza jeshi la nchi hiyo kuruhusu misaada ya kibinadamu kutoka Marekani.

Upinzani nchini Venezuela unapanga maandamano zaidi leo kushinikiza jeshi la nchi hiyo kuruhusu misaada ya kibinadamu kutoka Marekani, ambayo rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo anasema ni hatua za mwanzo za kufanya uvamizi dhidi ya taifa hilo. Kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa Rais wa taifa hilo Juan Guaido anatarajiwa kuongoza maandamano hayo mashariki mwa Caracas[…]

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ngazi ya klabu, Timu ya Simba ya DSM leo watakuwa Uwanja wa Taifa wakitafuta pointi muhimu mbele ya timu ya Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni wa mzunguko wa nne na mpaka sasa hakuna timu ambayo ina uhakika wa kwenda robo fainali kwenye kundi lao la D. Simba ipo Kundi D ikiwa na timu za Al Ahly iliyo kileleni na pointi saba, AS Vita ya CONGO DRC yenyewe ni[…]

Serikali kupitia Wizara ya Maji imepanga kutoa shilingi bilioni moja kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mkoa wa Iringa (IRUWASA) kwa ajili ya upanuzi wa miradi mbalimbali ya maji mkoani humo kama sehemu ya juhudi za serikali kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji.

Akiwa katika ziara ya siku 5 mkoani Iringa, Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani humo, amesema serikali imepanga kutumia bilioni moja kwa IRUWASA ili kuboresha huduma za upatikanaji wa maji kama sehemu ya mkakati wa serikali kutoa msukumo katika sekta hiyo. Kwa upande wake Mkuu[…]

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Japhet Mengele amekiri kuwa serikali imesikiliza kilio cha wananchi wa Njombe kwa kufanyia kazi utekaji na mauaji ya watoto wadogo yaliyoshika kasi katika siku zilizopita mkoani Njombe.

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Japhet Mengele amekiri kuwa serikali imesikiliza kilio cha wananchi wa Njombe kwa kufanyia kazi utekaji na mauaji ya watoto wadogo yaliyoshika kasi katika siku zilizopita mkoani Njombe. Mauaji hayo yameonekana kuchafua taswira ya mkoa wa Njombe kwa kuhusishwa na imani za kishirikina, jambo ambalo serikali[…]