Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo wakati akitoa muhtasari wa yaliyojiri kwenye Mkutano wa 32 wa Wakuu wa nchi za Afrika (AU) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopa. Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo amesema katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Serikali barani Afrika zimesisitizwa kupambana na wala rushwa, ambapo Tanzania imetajwa[…]

Mamia ya watumiaji wa barabara ya Mbalizi-Mkwajuni mkoani Songwe wamekwama kuendelea na safari zao baada ya mto Ngumba kufurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Mamia ya watumiaji wa barabara ya Mbalizi-Mkwajuni mkoani Songwe wamekwama kuendelea na safari zao baada ya mto Ngumba kufurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo huku msafara wa mkuu wa mkoa wa songwe ukikwama kwa zaidi ya saa nne. Msafara huo ulikatika kutokana na mvua za masika kunyesha mfululizo na kupelekea msafara wa Mkuu[…]

Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya uongozi nchini, imewakutanisha wadau wa sekta ya madini kujadili kanuni za Sheria ya madini ya mwaka 2017, ili rasilimali hiyo iweze kuwanufaisha Watanzania.

Katika kikao hicho kinachoketi Jijini Mwanza, shabaha kubwa inalenga kuimarisha soko la Madini, ili rasilimali hiyo iweze kuchangia kikamilifu katika pato la Taifa, baada ya kubainika kuwa bado kuna wimbi kubwa la utoroshaji wa madini hapa nchini. Kutokana na mjadala huo inategemewa kuwa, hii itakuwa ni neema kwa wachimbaji wadogo pia kupata soko la uhakika,[…]

Watanzania wametakiwa kuwa tayari kwa mabadiliko makubwa ya mwonekano wa jiji la Dar es salaam, kufuatia mpango kabambe wa jiji hilo.

Watanzania wametakiwa kuwa tayari kwa mabadiliko makubwa ya mwonekano wa jiji la Dar es salaam, kufuatia mpango kabambe wa jiji hilo ambao unaweka mikakati ya maendeleo ya eneo la jiji pamoja na maeneo yanayozunguka kwa kipindi cha miaka 20 kuanzia mwaka 2016- 2036. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam ambaye[…]

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini DSM ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.75.

Katika kesi hiyo Wambura anakabiliwa na shtaka moja la kughushi, Shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha. Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali George Barasa akisaidiana na Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin[…]

Watuhumiwa wawili wa Ujambazi wameuwawa katika tukio la kurushiana risasi na jeshi la polisi eneo la Pugu Mnadani baada ya watuhumiwa hao kutaka kufanya jaribio la uporaji.

Watuhumiwa wawili wa Ujambazi wameuwawa katika tukio la kurushiana risasi na jeshi la polisi eneo la Pugu Mnadani baada ya watuhumiwa hao kutaka kufanya jaribio la uporaji ambalo lilivurugwa na kikosi maalum cha kupambana na ujambazi cha jeshi hilo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar[…]

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May anakusudia kuliomba bunge la nchi yake limpe muda zaidi ili aweze kufanya mazungumzo na Umoja wa Ulaya juu ya kuubadilisha mkataba wa Brexit uliopo sasa.

Kufuatia kauli hiyo hivyo sasa Bi Theresa May anatarajiwa wiki ijayo kutoa taarifa bungeni juu ya hatua aliyofikia kwenye mazungumzo anayofanya na Umoja wa Ulaya. Zikiwa zimesalia siku 47 kwa nchi hiyo kuondoka Umoja wa Ulaya Waziri wa masuala ya jamii, James Borokenshire amesema kwamba bunge linatakiwa kupitisha maamuzi kuhusu mpango huo wa May, hadi[…]

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Raymond Mangwala amewataka vijana nchini kuona fahari na kuwa mabalozi wazuri wa maendeleo ya kiuchumi yaliyofikiwa katika kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya 5.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Raymond Mangwala amewataka vijana nchini kuona fahari na kuwa mabalozi wazuri wa maendeleo ya kiuchumi yaliyofikiwa katika kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli badala ya kukaa kimya na hivyo kutoa mwanya kwa baadhi ya watu[…]

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema serikali itatoa Shs Milioni 139 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji katika kata ya Kansai wilayani Karatu ambao umekwama kwa muda mrefu.

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema serikali itatoa Shs Milioni 139 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji katika kata ya Kansai wilayani Karatu ambao umekwama kwa muda mrefu ili uwaondolee wananchi tatizo kubwa la maji linalowakabili. Polepole ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi huo na kukuta bado haujakamilika ambapo[…]