Wakurdi nchini Iraq wamepiga kura leo katika uchaguzi wa bunge wa eneo linalojitegemea la Kurdistan, ikiwa ni mwaka mmoja tokea eneo hilo lilipofanya kura ya maoni ya kutaka kujitenga

Wakurdi nchini Iraq wamepiga kura leo katika uchaguzi wa bunge wa eneo linalojitegemea la Kurdistan, ikiwa ni mwaka mmoja tokea eneo hilo lilipofanya kura ya maoni ya kutaka kujitenga iliyoshindikana na kuikasirisha serikali kuu ya Iraq. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi na vilitarajiwa kufungwa saa kumi na mbili jioni. Watu wapatao milioni[…]

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na matetemeko makubwa ya ardhi pamoja na Tsunami nchini Indonesia imeongezeka na kufikia jumla ya watu 832

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na matetemeko makubwa ya ardhi pamoja na Tsunami katika kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia imeongezeka na kufikia jumla ya watu 832 kwa mujibu wa repoti za hivi karibuni. Idadi hiyo iliyotangazwa na shirika la maafa la taifa imeongezeka maradufu kuliko ile iliyotangazwa awali ambapo Makamu wa rais wa Indonesia[…]

Serikali imewahakikishia wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma uhakika wa masoko ya zao hilo kutokana na kilio cha wao kukosa masoko

Serikali imewahakikishia wakulima wa zao la zabibu mkoani Dodoma uhakika wa masoko ya zao hilo kutokana na kilio cha wao kukosa masoko hali inayoathiri ukuaji wa kipato cha wakulima na taifa kwa ujumla. Akiwa katika ziara ya kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji wa zabibu katika mashamba yaliyopo kata ya Hombolo Jijini Dodoma, Mkuu wa[…]

Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kesho inataraji kufungua Dawati la Mnyororo wa Biashara za Mifugo na Uvuvi Nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha mazao yatokanayo na hizo yanaongezeka

Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kesho inataraji kufungua Dawati la Mnyororo wa Biashara za Mifugo na Uvuvi Nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha mazao yatokanayo na hizo yanaongezeka na kuwanufaisha wananchi na nchi kwa ujumla. Wakizungumza na kituo hiki jijini Dodoma, Makatibu Wakuu wa Wizara hiyo ya Mifugo na Uvuvi wameweka wazi kuwa kufunguliwa kwa dawati[…]

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,amesema,Serikali ya awamu ya tano iliyochini ya Rais Dkt Magufuli imejipanga kikamilifu kushughulikia kero zote za kijamii, zikiwemo zinazohusiana na migogoro ya madini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,amesema,Serikali ya awamu ya tano iliyochini ya Rais Dkt John Magufuli imejipanga kikamilifu kushughulikia kero zote za kijamii, zikiwemo zinazohusiana na migogoro ya madini na kuyataka mabenki kote nchini kuanzisha kitengo maalumu cha kupokea Madini ya dhahabu. Mbali na hilo,pia amesema Serikali imeshaunda tume kuchunguza maeneo yote yenye reseni za uchimbaji madini[…]

Kuelekea mechi ya Simba na Yanga kesho Septemba 30 2018, TFF imesema haitaruhusu mtu yoyote kuwepo nje ya Uwanja huo bila tiketi

Hatua hiyo imekuja mara baada ya shirikisho hilo kutangaza zoezi la kuanza kuuzwa kwa tiketi hizo Septemba 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Clifford Ndimbo, amesema hakutakuwa na uuzwaji wa tiketi nje ya Uwanja wa Taifa siku ya mechi ili kuepusha vurugu na usumbufu. Ndimbo ameeleza kwa kesho tiketi zitakuwa zinauzwa chuo[…]

Serikali imetoa wito kwa makampuni ya ndani na ya nchi kutumia huduma za makampuni ya matangazo ya ndani ili yaweze kukua kibiashara

Serikali imetoa wito kwa makampuni ya ndani na ya nchi kutumia huduma za makampuni ya matangazo ya ndani ili yaweze kukua kibiashara na kutoa mchango wa kukuza uchumi wa nchi. Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Jenista Mhagama ametoa wito huo jijini DSM na kusema makampuni ya[…]

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango ameuagiza uongozi wa TRA kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu wafanyakazi wake wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo rushwa

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu wafanyakazi wake wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo rushwa na kutumia njia zisizokubalika wakati wa kukusanya kodi za Serikali. Dkt. Mpango ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa[…]

Idadi ya watu waliokufa kutokana na matetemeko mawili ya ardhi yenye nguvu ya Tsunami nchini Indonesia imeongezeka na kufikia watu 384.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa maafisa wa idara inayoshughulikia maafa nchini Indonesia. Wakati huo huo mamia ya watu waliojeruhiwa wanapata huduma hospitalini huku waokoaji wakiendelea kujitahidi ili kulifikia eneo hilo lililoathirika. Hadi sasa, vifo vyote vilivyoorodheshwa ni kutoka katika eneo la Palu lililokumbwa na tsunami, siku moja baada ya mawimbi makubwa ya kiwango cha[…]

Serikali imeshauriwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabara ili iweze kwenda sambamba na mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika sekta ya nishati ya umeme

Serikali imeshauriwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabara ili iweze kwenda sambamba na mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika sekta ya nishati ya umeme ambayo yameleta tija katika uzalishaji viwandani kwani kwa sasa nishati hiyo inatosheleza mahitaji ikilinganishwa na awali. Ushauri huo umetolewa jijini Dsm na Meneja kitengo cha umeme kiwanda cha saruji Camel Rashid Ukondwa, alipotembelewa na shirika[…]