Kaimu mtendaji na M/kiti wa mtaa Msalala wilayani Temeke wamejikuta matatani kwa hili

screen-shot-2017-01-11-at-4-07-57-pm

Kaimu mtendaji wa kata ya Makangarawe wilayani Temeke jijini Dsm Peter Mwang’onda pamoja na mwenyekiti wa mtaa msalala wilayani temeke wamejikuta matatani baada ya Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kutoa amri ya kuhojiwa na Polisi kuhusu Upotevu wa shilingi Million 3 zilizotolewa na manispaa ya Temeke kwa ajili ya ukarabati wa barabara katika mtaa huo.

Akizungumza na wananchi katika kata ya makangarawe Temeke jijini Dsm wakati akisikiliza kero mbali mbali za wananchi Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva amesema serikali haitosita kuchukua hatua kali dhidi ya watumishi wa Umma ambao wanakikuka maadili kwa kujihusisha na wizi au ubadhilifu katika miradi ya wananchi.

Aidha katika mkutano huo amewataka wenyeviti wote wa mitaa wilayani temeke kukabidhi mihuri kwa watendaji wa mitaa kutokana na baadhi yao kuitumia vibaya kwa kujinufaisha binafsi,ambapo pia ametoa maagizo ya kuandikishwa wakazi wote wilayani Temeke pamoja na wageni wanaoingia katika daftari la kudumu ili kuwatambua ili kupambana na matukio ya uhalifu.

Mkuu wa wilaya yupo katika ziara wilayani Temeke kukagua maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo yatakayopita mradi wa kuboresha wilaya hiyo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa DMDP.

Facebook Comments