Mapambano dhidi ya Ujangili Katibu Mkuu awataka watumishi wajipange Morogoro

screen-shot-2017-01-11-at-3-03-03-pm

Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudensi Milanzi amewataka watumishi wa Maliasili na Utalii kujipanga kikamilifu ili kukabiliana na ujangili na kuleta mabadiliko katika utendaji kazi bila kumuonea huruma atekayekwenda kinyume na maadili ya uhifadhi.

Akiongea na mameneja wa wanyamapori na na wajumbe wabodi ya wanyamapori mkoani Morogoro katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Gaudensi Milanzi amewataka wafanyakazi wote wa maaliasili kujipanga zaidi kukabiliana na ujangili unafanywa na baadhi ya watu wachache wakilenga kuhujumu uchumi wa taifa.

Aidha kwa kipindi cha mwaka 2015 zaidi ya watu 200 wamefungwa gerezani kwa makosa ya kupatikana na nyara za serikali ambapo kiasi cha shilling bilioni 164 zilitemewa kukusanywa kutokana na faini ya makosa hayo.

Facebook Comments