Nyumba 200 kuvunjwa Kigogo Wakazi wapewa notisi baada ya kushindwa kesi

screen-shot-2017-01-11-at-6-00-24-pm

Wakazi wa eneo la Kigogo kati jijini Dar es salam wameiomba Serikali kuingilia kati na kuzuia utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Mwanzo Ilala ya kuondoa zaidi ya nyumba mia mbili za makazi ya watu zilizopo eneo la RANDA BAR SHAMBA LA PIPO Kigogo kwa madai kuwa zimejengwa ndani ya eneo la mtu, ambapo tayari wamepewa notice ya siku 14 ya kutakiwa kuondoka katika eneo hilo ili kupisha zoezi la uvunjwaji wa nyumba hizo.

Wakizungumza na Channel Ten wakazi hao wamedai kushangazwa na uamuzi huo kwani awali ilidaiwa kuwa wamevamia eneo la kiwanja cha mpira lakini baadaye ikaelezwa ni eneo la mtu aliyetajwa kuwa SUNGURA KHAMIS ambaye baada ya kufungua shauri mahakamani amepewa haki ya kuwaondoa, hivyo wanaiomba Serikali kuzuia utekelezaji wa shauri hilo kwani baadhi yao wanavyo vibali halali vya kuwaruhusu kujenga na hata Serikali inawatambua kama wakazi halali.

Uongozi wa Serikali ya mtaa Kigogo kati umekiri kupokea notisi ya kuvunjwa nyumba zaidi ya 200 katika eneo hilo ifikapo Ijumaa wiki hii kwa madai ya kuwa wakazi hao walivamia na kujenga kwenye kiwanja ambacho ni mali ya mtu.

Juhudi za kumpata mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo hazikufanikiwa mara moja.

Facebook Comments