Rais Magufuli awasili Simiyu asisitiza kutotoa chakula cha Msaada

screen-shot-2017-01-11-at-2-52-01-pm

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada huku akiwahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha masanza kona wilayani busega mara baada ya kuwasili akitokea mkoani mwanza rais magufuli amewashukuru wananchi kwa kumchagua oktoba 25 mwaka 2015 na kuahidi kutatua matatizo yanayowakabili yakiwemo ya maji na umeme .

Aidha amesisitiza kutotoa chakula cha msaada kwa wananchi na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii sambamba na kulima mazao yanayostahimili ukame kama vile mtama ,viazi na ufuta.

Rais magufuli ameahidi kutafuta fedha kwaajili ya kukamilisha kilomita 50 kwa kiwango cha lami kutoka bariadi mjini hadi maswa baada ya kukamilika kwa barabara ya lamadi bariadi yenye urefu wa km 72.8.

Facebook Comments