Wadau wa habari wakiongozwa na MCT leo wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari

screen-shot-2017-01-11-at-4-01-00-pm

Wadau wa habari wakiongozwa na Baraza la habari Tanzania MCT leo wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari namba 12 ya mwaka 2016 katika mahakama ya Afrika Mashariki EACJ jijini Dar es salaam.

Katibu mtendaji baraza la habari Tanzania MCT Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kesi hiyo mahakamani hapo amedai kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania novemba 5 mwaka jana ina baadhi ya vifungu ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza.

Akielezea sababu ambazo zimepelekea wao kufungua kesi katika mahakama ya Afrika ya Mashariki mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Fulgence Massawe anafafanua.

Wadau wengine wa habari na watetezi wa haki za binadamu nchini wameungana na Baraza la habari Tanzania katika kufungua kesi hiyo ya kupinga sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.

Hivi sasa wadau mbalimbali wa habari nchini wamemaliza kupeleka mapendekezo ya kanuni za sheria hiyo ya huduma za vyombo vya habari ambazo ziko chini ya mamlaka ya waziri wa habari.

Facebook Comments