Agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa alilo litoa wilayani Karatu

kassim-majaliwa-1

Serikali mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi katika utekelezaji wa agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa alilo litoa wilayani Karatu katika bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa mashine za kuvuta maji umbali wa mita 500 kutoka chanzo cha maji katika bonde hilo linalo tumika kwa kilimo cha Mazao mbalimbali.

Katika agizo Lake, waziri mkuu, aliagiza kusogezwa kwa mashine za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo wakati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali wa mita 60 kwa sheria ya mazingira.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wazee, viongozi wa dini na wakuu wa idara ya halmashauri ya wilaya ya Karatu katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi wilayani humo anasema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa chakula haikuwa busara kuchoma mashine zile bila kujali mazao ambayo tayari yameoteshwa katika eneo hilo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi hao wanasema pengine ushirikishwaji wa wananchi wa eneo hilo haukuzingatiwa.

Na je nini sasa msimamo wa serikali katika kumaliza mvutano huo?

Gambo yupo katika ziara ya kikazi wilayani KARATU ambapo atakagua na kutembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali kusikiliza kero zao.

Facebook Comments