Shambulio la uwanja wa ndege Marekani Mshambuliaji akikutwa na hatia kunyongwa

screen-shot-2017-01-08-at-4-44-22-pm

Maafisa nchini Marekani, wamemshitaki mwanajeshi wa zamani aliyewaua watu watano na kuwajeruhi wengine sita kwa kuwapiga risasi katika uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale, usiku wa kuamkia jana.

Esteban Santiago mwenye umri wa miaka 26 na ambaye alihudumu kama mlinzi nchini Iraq kabla ya kuachishwa kazi kufuatia utendaji usioridhisha, anakabiliwa na mashitaka ya ukiukaji wa sheria za bunduki na kufanya kitendo cha vurugu.

Mwendesha mashtaka wa Marekani Wilfred Ferrer amesema ikiwa Santiago atapatikana na hatia, basi anaweza kuhukumiwa kifo, au kifungo cha maisha gerezani. Santiago aliyetokea Alaska, alichomoa bunduki yake alipokuwa katika eneo la kupokea mizigo, na kuwapiga watu risasi. Risasi zilipoisha alijiangusha kifudifudi ndipo akakamatwa.

Facebook Comments