Vladmiri Putin Aliamuru udukuzi dhidi ya Hillary Clinton

putin

Urusi imepinga shutuma kuwa Rais wa nchi hiyo Vladmir Putin,aliamuru ufanyike udukuzi,dhidi ya Hillary Clinton na Chama chake cha Democratic,kumsaidia Donald Trump,kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Andrey Klimov,ambaye ni makamu mwenyekiti wa Seneti inayoshughulika na uhusiano wa kimataifa,amesema,Urusi ni tishio na imekuwa ikisakamwa kwa maneno mabaya huku Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Klemlin,ikifananishwa na shetani.

Bwana Klimov,amesema,Urusi haikuwa na sababu za kufanya hivyo licha ya kwamba ilimuona Hillary Clinton, kuwa tishio kwa sera zake za nje lakini hakusita kusema kuwa hawakufikiria hata kidogo kuwa Trump atashinda uchaguzi huo.

Wakati huo huo chombo kimoja cha habari nchini Marekani,kimesema,hakielewi safari hii Rais Putin,ana malengo gani, kufuatia miongo miwili sasa kuweza kucheza na akili za maraisi watatu wa nchi hiyo ,Billy Clinton,George W Bush,Barack Obama na mteule Donald Trump.

Facebook Comments