Vita dhidi ya Ugaidi Marekani yamsaka mtoto wa Osama bin Laden

screen-shot-2017-01-06-at-6-19-07-pm

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imetangaza kutoa zawadi ya dola milioni 5 kwa atakayesaidia kukamatwa kwa mtoto wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa zamani wa kikundi Al Qaeda Osama bin Laden bwana ambae kwa sasa anatajwa kuwa ndiye kiongozi mkuu wa kikundi hicho.

Taarifa kutoka katika wizara hiyo imemtaja Hamza Bin Laden katika orodha ya magaidi akiwa katika umri wa miaka ishirini amekuwa kiongozi wa kundi hilo ambalo liliasisiwa na baba yake mzazi

Katika orodha hiyo ya magaidi pia ametajwa kiongozi mkuu wa usalama wa Al qaeda Ibrahim al-Banna huku Hamza Bin Laden akitangaziwa kuwekewa vikwazo vya kufanya biashara na wamarekani pamoja na mali zakekuzuiliwa.

Imetajwa kuwa Hamza Bin Laden amekuwa makini katika suala hilo kwa kufuata nyayo za baba yake kwa kujiunga na jihadi na kusambaza ujumbe wa sauti kwa niaba ya kundi la Al Qaeda na kuchochea mashambulizi dhidi ya nchi za Magharibi.

Facebook Comments