Mpango mkubwa wa Biashara barani Asia Tanzania yaingizwa kwenye mpango

samia

Jitihada za Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan za kuiingiza Tanzania kwenye mpango mkubwa wa Biashara barani Asia, Mashariki ya kati, Ulaya na Afrika umefanikiwa baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi Saba kuingizwa katika mpango unaojulikana kama China One Belt, One Road Strategy.

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais imebainisha nchi nyingine zilizochaguliwa kuingizwa kwenye mpango huo ni Malaysia, Sri Lanka, Nepal, Bangladesh, Pakistan na Thailand.

Baada ya Tanzania kuingizwa rasmi katika mpango huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amekutana na Watendaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Biashara (TCCIA) na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuwaeleza kuhusu muhimu wa Tanzania kuingizwa kwenye mpango huo.

Baada ya kuingia kwenye mpango huo, Tanzania itanufaika na fedha za mfuko kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ambazo zinatolewa kwa nchi zilizojiunga na mpango huo.

Facebook Comments