Umoja wa masoko DSM umeiomba serikali kuboresha masoko yote ili yaweze kuendana na hadhi ya mkoa

soko

Umoja wa masoko mkoa wa Dar es salaam umeiomba serikali kuboresha masoko yote yaliyopo mkoani humo ili yaweze kuendana na hadhi ya mkoa kwani majengo na miundombinu ya masoko hayo ni chakavu.

Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti wa masoko mkoa wa dsm Mohamed Mwekya ambapo amesema masoko ya dsm yamechakaa ukilinganisha na mikoani huku akisisitiza kuwa viongozi wawainue wafanyabishara kwa kuboresha maeneo yao lakini pia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ikiwemo kuwatafutia namna nzuri ya kukopeshwa ili kukuza mitaji yao.

Bw. Mwekya amemkumbusha mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda kufuatilia suala la mipaka ya soko la Tandale ambalo waliahidiwa kuwa litafanyiwa kazi wakati waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI George Simbachawene alipofika sokoni hapo kwa ajili ya kufanya usafi huku mkuu wa mkoa wa sasa akiwa mkuu wa wilaya ya kinondoni.

Facebook Comments