Watu wanane wauawa Somalia Katika mashambulizi ya kujitoa muhanga

78b14abb24cd4894b89815fcf9bdb3fc_18

Watu wanane wameuawa katika mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga yaliyoilenga kwa wakati unaokaribiana hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Habari zinasema kuwa bomu la kwanza la gari limeripuka kwenye kizuizi cha barabarani karibu ya uwanja wa ndege na kuwauwa maafisa kadhaa wa usalama, na baadaye kidogo lori likapita kwa kasi katika kizuizi hicho, na kuripuka karibu ya Peace Hotel, ambayo inapendelewa zaidi na watalii pamoja na maafisa wa serikali.

Mripuko huo umeiharibu sehemu moja ya jengo la hoteli hiyo ambapo kundi la itikadi kali za kiislamu, al-Shabab ambalo linapigana kuiondoa madarakani serikali inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, limedai kuhusika na shambulio hilo.

Facebook Comments