TCRA yatishia kufuta makampuni mawasiliano nchini yasiyojisajili

screen-shot-2017-01-03-at-5-59-54-pm

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema haitasita kuchukua hatua za kisheri ikiwemo kusitisha ama kufuta leseni ZA Makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano nchini ambayo hayatajisajili kwenye soko la Hisa la Dar es salaam DSE kufuatia kumalizika kwa muda wa usajili uliowekwa awali na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na dhamana CMA.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandshi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kulaba amsema muda wa tarehe ya mwisho ya usajili kwa makampuni hayo katika soko la hisa ilikuwa ni Desemba 31 ambapo kwa mujibu wa TCRA ilipeleka majina 89 ya makampuni mbalimbali yanayotoa huduma za Mawasiliano hapa nchini lakini kwa mujibu wa DSE, mpaka sasa ni makampuni matatu tu ndiyo yaliyokwishajisajili DSE ambayo Vodacom, Tigo na Airtel.

Kwa mujibu wa TCRA hatua hizo za kisheria dhidi ya makampuni hayo zitaanza mara moja baada ya taarifa za uhakiki wa makampuni 89 kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana CMA kukamilika.

Facebook Comments