Harufu ya soko la Shekilango limelalamikiwa kutokana na uchafu uliokithiri

soko-la-shekilango

Soko la Shekilango lililoko Sinza jijini Dar es salaam limelalamikiwa kutokana na uchafu uliokithiri katika soko hilo ambao umepelekea kuwepo na harufu kali katika eneo hilo ambayo imekuwa kero kwa watumiaji wa soko hilo pamoja na watu mbalimbali wanaotumia barabara za Shekilango na Morogoro.

Camera ya Chnnel Ten ilifika katika soko hilo na kujionea hali halisi huku kukiwa na harufu kali inayodaiwa kutokana na eneo la machinjio ya kuku yaliyopo ndani ya soko hilo ambayo yanadaiwa kutofanyiwa usafi ipasavyo mara baada ya shughuli za uchinjaji na uhifadhi mbovu wa taka hizo ambao ndio unaodaiwa kuzalisha harufu kali sokoni hapo.

Channel Ten ilifanya mahojiano na wafanyabishara pamoja na watumiaji wa soko hilo ambapo wamesema hali hiyo imekuwa ni kero kwao na imekuwa ikipunguza idadi ya wateja wanaofika sokoni hapo kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali kutokana na harufu huku pia ikiushangaa uongozi wa soko hilo kushindwa kuweka utaratibu wa kufanya usafi kila siku licha ya ushuru ambao wafanyabishara wamekuwa wakitozwa na uongozi huo…

Aidha wafanyabishara hao wameutaka uongozi wa soko hilo kuhakikisha kunakuwa na ratiba za usafi za kila siku na sio kusubiria baada ya siku tatu kama wanavyofanya kila siku ikiwemo kutumia madawa ya usafi kila siku yatakayosaidia kuondoa harufu kali sokoni hapo ambapo sio tu imekuwa kero kwa wafanyabishara na wateja bali pia hata kwa wakazi wanaoishi hilo la soko la Shekilango…

Baada ya malalamiko hayo Channel Ten ilibisha hodi katika ofisi za Uongozi wa Soko hilo la Shekilango zilizopo sokoni hapo na kukutana na Mwenyekiti wa soko hilo David Mrisho ambae alikiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo uongozi umeshindwa kulitatua licha ya kujaribu bila mafanikio.

Facebook Comments