Kocha Wenger apuuza wanaomkosoa Asema ni utamaduni mbaya, asisitiza Arsenal itabaki imara

screen-shot-2016-12-27-at-10-50-26-am

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ukosoaji unaoendelea dhidi yake kwa sasa umepita kiasi, hasa wakati ambapo timu yake inaendelea kuimarisha harakati zake za kushinda taji la ligi kuu.

Gunners wako katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 37, ambazo ni tisa chini ya vinara Chelsea.

Wenger akiwa katika msimu wake wa 20 na Arsenal amelifananisha soka na siasa katika jamii akisema kila mtu ana maoni yake.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa ,ambaye kandarasi yake inakamiika mwishowe wa msimu huu amesema kuwa anaendelea kujiuliza kila mara.

Facebook Comments